Umri wa miaka 18 au zaidi pekee. Inapatikana kwa watumiaji walio na umri wa miaka 18 na zaidi.
Google Flow Music ni studio ya muziki ya AI kutoka Google Labs inayorahisisha kutunga nyimbo kwa kutumia AI. Fafanua hali au ubandike maneno ya wimbo wako ili upate wimbo kamili wenye ubora wa juu. Kisha uendelee kuuboresha ukitumia zana yako ya kutayarisha muziki inayotumia AI hadi uwe jinsi unavyotaka.
Hutahitaji chumba cha kurekodia, vifaa wala ujuzi wa nadharia ya muziki. Iwe unaandika wimbo wako wa kwanza au umekuwa ukitayarisha midundo kwa miaka mingi, Flow Music hukusaidia kutayarisha muziki kwa urahisi.
GEUZA HALI AU MANENO YA WIMBO YAWE WIMBO KAMILI
Andika kidokezo kama vile "nyumba yenye mwanga wa jua nikinywa kahawa yangu ya saa 1 asubuhi" au ubandike maneno ya wimbo uliyoandika kisha Flow Music itatayarisha wimbo kamili wenye urefu kamili ulio na sauti na ala. Jaribu aina yoyote: pop, hip-hop, lo-fi, house, indie rock, R&B, country na nyinginezo.
PIGA GUMZO NA ZANA YAKO YA KUTAYARISHA INAYOTUMIA AI
Boresha wimbo wako kwa kusema tu unachotaka. Iombe Zana yako ya kutayarisha, inayotumia Gemini, "iongeze besi," "iweke gitaa ya pekee kwenye kiunganishi" au "iimbe kwa sauti nzito." Hutekeleza mabadiliko na kuendelea kuboresha wimbo wako, hatua kwa hatua.
TOLEO JINGINE LA WIMBO, KUBADILISHA NA KUREFUSHA
Pakia nyimbo zako au uandae miseto ya nyimbo ulizotayarisha. Tayarisha toleo lingine la wimbo katika muundo mpya, badilisha sehemu (badilisha gitaa uweke kinanda chenye sauti tulivu cha Rhodes) au uongeze urefu wa wimbo kwa kuweka ubeti au sehemu mpya ya mwisho.
TAYARISHA VIDEO YA MUZIKI YA WIMBO WAKO
Fanya wimbo wako upendeze zaidi ukitumia video ya muziki ya AI iliyotayarishwa kwa Veo, mfumo wa kubuni video wa Google. Elekeza mwonekano, wahusika na hali, kisha utume video iliyosawazishwa na wimbo wako.
TAYARISHA UKITUMIA UBUNIFU
Piga hatua zaidi ukitumia Ubunifu: tayarisha programu jalizi maalum za sauti, michezo ya muziki au programu zako ndogo za muziki. Watumie wengine ili waweze kuzitumia na kuandaa miseto.
TUMA NA UGUNDUE MUZIKI
Chapisha nyimbo zako, tayarisha orodha, fuatilia watayarishi na ugundue muziki mpya kila siku. Flow Music hujifunza mapendeleo yako unapotayarisha, kwa hivyo inakaribia mapendeleo yako binafsi ya muziki kadiri muda unavyosonga.
Tafuta mapendeleo yako ya muziki ukiwa msanii au mtayarishaji mpya. Tumia Flow Music kama mfumo wako wa AI wa kutayarisha nyimbo ili utayarishe wimbo wa siku ya kuzaliwa ya rafiki, wimbo mkuu wa podikasti yako, mdundo wa video yako ijayo au wimbo unaokufaa. Utatayarisha nini leo?
Sheria na Masharti: https://policies.google.com/terms
Sera ya Faragha: https://policies.google.com/privacy
Ilani ya Faragha: https://www.flowmusic.app/privacynotice
Studio yako ya muziki ya AI: Geuza wazo au maneno kuwa nyimbo, miseto na video.
Ilisasishwa tarehe
25 Nov 2026